• Home
  • About us
  • Contact us
  • Privacy Policy

Tanzaniayetu.com

    • Habari
    • Michezo
    • Urembo
    • Mahusiano
    • Burudani
    • Teknolojia
    • Kilimo
  • Breaking News

    Home / Unlabelled / Rais Dkt. Samia kuisuka upya Muhimbili kwa TZS 1.2 Trilioni

    Rais Dkt. Samia kuisuka upya Muhimbili kwa TZS 1.2 Trilioni

    Tanzania Yetu March 06, 2025

    Serikali imenunua na kusimika mtambo wa kisasa wa Angio-Suite Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) uliogharimu TZS. 2 Bil. Hivyo kuiwezesha hospitali kutoa matibabu ya ubingwa bobezi ambayo yalikua hayapatikani hapa nchini hivyo kuongeza idadi ya aina za matibabu ya kibobezi katika eneo hilo ambapo takribani wagonjwa 2,300 wamehudumiwa tangu mtambo huo ulipofungwa mwishoni mwaka 2022.

    Akiwasilisha taarifa ya mafanikio ya MNH kwa kipindi cha miaka minne chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji Dkt. Rachel Mhaville aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo amesema, kupitia mtambo huo kwa mara ya kwanza nchini hospitali imefanikiwa kuanzisha huduma mpya mbalimbali ikiwamo kuweka mirija myembamba (catheters) kwa kutumia matundu madogo, kutoa damu iliyoganda katika mishipa ya damu pamoja na huduma nyinginezo ambazo zinafanyika kwa ustadi wa hali ya juu.

    Dkt. Mhaville ameeleza kuwa mbali na mtambo huo, pia Serikali imenunua mashine mpya ya Mammography iliyogharimu TZS. 1.8 Bil. ambayo ina uwezo wa kupima na kutoa picha zinazoweza kugundua uvimbe kwenye matiti ukiwa katika hatua za awali kabisa ambapo wagonjwa 810 wamehudumiwa tangu mashine hiyo iliponunuliwa mwaka 2024.

    “Mashine hii ya Mammography ni ya kisasa na pekee kwa Hospitali za Umma, inatumiwa na madaktari wabobezi wa radiolojia ya wanawake na imeleta mapinduzi katika utoaji wa huduma za uchunguzi wa kisasa kwa wenye magonjwa ya saratani ya matiti, amesisitiza Dkt. Mhaville.

    Vilevile katika kipindi tajwa, Serikali imeongeza mashine moja yenye nguvu sumaku 1.5T ambayo inaweza kuona uvimbe mdogo kwenye picha za uchunguzi, iliyogharimu TZS. 2.6 Bil. hivyo kuondoa muda wa wagonjwa kusubiri kutoka siku 4 hadi 5 za awali kufanya kipimo hicho na kufanyika siku hiyohiyo aliyoandikiwa mgonjwa. Ongezeko la mashine ya Kidigitali ya X-Ray iliyogharimu kiasi cha TZS. 358 Mil. imefanikisha hospitali kupunguza muda wa kutoa majibu ya radiolojia kutoka ndani ya saa 48 hadi 24 tangu kipimo kilipofanyika.

    Amesema kuwa, Serikali imeongeza mashine moja ya CT-Scan (dual) iliyogharimu TZS. 1.8 Bil. yenye uwezo wa vipande 128 hivyo kuongeza idadi ya wagonjwa wanaopimwa kwa siku kutoka 20 hadi zaidi ya 50 na majibu kupatikana kwa haraka, kumwezesha daktari kufanya maamuzi mapema na wagonjwa kupata matibabu stahiki kwa wakati.

    “Vilevile hospitali imefanikiwa kununua vifaa vingine ikiwamo mashine za kusadia wagonjwa kupumua 18 zilizogharimu TZS. 932 Mil, mashine za endoskopia zilizogharimu TZS. 215, vifaa vya maabara TZS. 1.8 Bil hatua iliyowezesha uboreshaji mkubwa wa huduma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ameongeza Dkt. Mhaville.

    Rais Dkt. Samia kuisuka upya Muhimbili kwa TZS 1.2 Trilioni Rais Dkt. Samia kuisuka upya Muhimbili kwa TZS 1.2 Trilioni Reviewed by Tanzania Yetu on March 06, 2025 Rating: 5
    Share This
    Facebook Twitter Google+

    No comments

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    Tanzania Yetu

    Tanzania Yetu

    The Africa Energy Summit - Mission 300

    The Africa Energy Summit -  Mission 300
    The Africa Energy Summit - Mission 300

    Contacts Details

    tanzaniayetugazeti@gmail.com

    Recent on trending

    • HUYU NDIYE SAID LUGUMI, HISTORIA YAKE YA KWELI
      HUYU NDIYE SAID LUGUMI, HISTORIA YAKE YA KWELI
        Bilionea Saidi Lugumi sio jina geni Nchini, huyu sio mtoto wa mjini, sio Kiongozi na huenda kwenye familia yake hakuna historia ya mwana...
    • AJALI YA LORI YAUWA MASHUHUDA 11, MAJERUHI 13 TANGA
      AJALI YA LORI YAUWA MASHUHUDA 11, MAJERUHI 13 TANGA
        Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga watu mashuhuda wa aja...
    • SERENGETI BYTES YATOA ORODHA YA WATANZANIA 100 WALIOCHOCHEA MABADILIKO KATIKA MWAKA 2024
      SERENGETI BYTES YATOA ORODHA YA WATANZANIA 100 WALIOCHOCHEA MABADILIKO KATIKA MWAKA 2024
        Kampuni ya Serengeti Bytes imetangaza rasmi toleo la pili la jarida la Watanzania 100 Wanaochochea Mabadiliko (100 Tanzanian Changemaker...
    • RAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA 'DR SAMIA SULUHU HASSAN GIRLS SEC. SCHOOL'
      RAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA 'DR SAMIA SULUHU HASSAN GIRLS SEC. SCHOOL'
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na ...
    •  Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Uzingatie Vipaumbele vya Wananchi - Naibu Waziri Kapinga
      Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Uzingatie Vipaumbele vya Wananchi - Naibu Waziri Kapinga
      Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Judith Kapinga amesema dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanashiriki...
    • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 30, 2024
      HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 30, 2024
      from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/3AgJSiV
    • Wimbo Mpya : NYANDA MALIGANYA - TAARIFA YA INAGA
      Wimbo Mpya : NYANDA MALIGANYA - TAARIFA YA INAGA
        from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/A9U1NO2
    • Gazeti la Tanzania Yetu, Januari 16 2025
      Gazeti la Tanzania Yetu, Januari 16 2025
    • UWEZO WA MITAMBO YA KUFUA UMEME WAFIKIA MEGAWATI 3,091.71- MHE.KAPING
      UWEZO WA MITAMBO YA KUFUA UMEME WAFIKIA MEGAWATI 3,091.71- MHE.KAPING
      - Wateja wapya 109,918 waunganishiwa na huduma ya umeme nchini - Kamati ya Bunge yaipongeza TANESCO kwa kuimarisha Miundombinu ya umeme Seri...
    • Nimeiacha CBE katika Mikono Salama: Prof. Anderson
      Nimeiacha CBE katika Mikono Salama: Prof. Anderson
      Na Georgina Misama, CBE. Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Wineaster Anderson amesema anaondoka katika nafasi hiy...

    Contact Form

    Name

    Email *

    Message *

    tanzania ytu

    tanzania ytu

    GAZETI LA TANZANIA YETU

    GAZETI LA TANZANIA YETU
    Gazeti la Kila Wiki

    Popular Posts

    • HUYU NDIYE SAID LUGUMI, HISTORIA YAKE YA KWELI
        Bilionea Saidi Lugumi sio jina geni Nchini, huyu sio mtoto wa mjini, sio Kiongozi na huenda kwenye familia yake hakuna historia ya mwana...
    • AJALI YA LORI YAUWA MASHUHUDA 11, MAJERUHI 13 TANGA
        Watu 11 wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa baada ya lori lililokuwa limebeba saruji kufeli breki na kugonga watu mashuhuda wa aja...
    • SERENGETI BYTES YATOA ORODHA YA WATANZANIA 100 WALIOCHOCHEA MABADILIKO KATIKA MWAKA 2024
        Kampuni ya Serengeti Bytes imetangaza rasmi toleo la pili la jarida la Watanzania 100 Wanaochochea Mabadiliko (100 Tanzanian Changemaker...
    • TUCTA: UWEKEZAJI KATIKA USALAMA NA AFYA UNALIPA
      Mkurugenzi wa Mafunzo,Utafiti, Takwimu, na Uhamasishaji wa OSHA, Bw. Joshua Matiko akiwasilisha mada juu ya masuala ya usalama na afya mah...
    • Gazeti la Tanzania Yetu, Januari 16 2025
    • UWEZO WA MITAMBO YA KUFUA UMEME WAFIKIA MEGAWATI 3,091.71- MHE.KAPING
      - Wateja wapya 109,918 waunganishiwa na huduma ya umeme nchini - Kamati ya Bunge yaipongeza TANESCO kwa kuimarisha Miundombinu ya umeme Seri...
    • Wimbo Mpya : NYANDA MALIGANYA - TAARIFA YA INAGA
        from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/A9U1NO2
    • RAIS SAMIA AZINDUA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA 'DR SAMIA SULUHU HASSAN GIRLS SEC. SCHOOL'
      Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mchepuo wa Sayansi na ...
    • Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Uzingatie Vipaumbele vya Wananchi - Naibu Waziri Kapinga
      Naibu Waziri wa Nishati na Mbunge wa Viti Maalum Vijana Taifa, Mhe. Judith Kapinga amesema dhamira ya Serikali ni kuona wananchi wanashiriki...
    • HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 30, 2024
      from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/3AgJSiV
  • Copyright © Tanzaniayetu.com