Watanzania watakiwa kulinda na kuitunza miundombinu ya treni ya SGR.
Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, amewasihi Watanzania kushirikiana na Shirika la Reli Tanzania (TRC), kuilinda na kuitunza miundombinu ya treni ya kisasa ya Umeme (SGR).
Prof. Mbarawa, ametoa wito huo katika stesheni ya Magufuli Dar es Salaaam, muda mchache baada ya kumsindikiza Rais wa Msumbiji Fransisco Chapo, aliyesafiri kwa SGR kutoka Stesheni ya Magufuli kwenda stesheni ya Pugu na kisha kurejea stesheni ya Magufuli, kwa lengo kushuhudia mradi huo ambao ni wa kilelezo barani Afrika.
Waziri wa Uchukuzi amesema Rais Chapo, aliyeko nchini kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu aliyoaianza Mei 07, 2028 ameeleza kufurahishwa na mradi huo aliosema ni wa kiwango cha dunia na kuwataka Watanzania, kuulinda kwa wivu.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa, alisema kuwa ujio wa Mhe. Chapo ni ishara tosha ya kwamba Afrika inajua nini kinachoendelea Tanzania na pia kuzidi kudumisha mahusiano baina ya nchi za Afrika na kuimarisha katika ufanyaji biashara kwa ukaribu.
“Kikubwa zaidi katika nchi za Afrika ni kufanya biashara na wenzetu wa nchi nyingine wanatutazama tofauti, na nchi ya Msumbiji tumekua tukishiriana katika Nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, ulinzi na vilevile kijamii ukizungumza mmakonde wa Msumbiji na Tanzania hawana tofauti” alisema Ndugu Kadogosa.
No comments