MAHAFALI YA 44 YA SHULE YA MSINGI MAPINDUZI “A”: WAHITIMU 79 WAPATA BARAKA NA AHADI ZA KUBORESHA SHULE

Mahafali haya yamehudhuriwa na viongozi wa shule, wazazi, walimu, wageni waalikwa, na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Mgeni rasmi, Mhe. Eustard Athanace Ngatale, aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma za Sheria OR-TAMISEMI, amekiri juhudi za walimu na wazazi katika kuhakikisha watoto wanapata elimu bora, akipongeza shule kwa kushika nafasi za juu kitaifa na kupewa heshima za kipekee.
“Ni fahari kubwa kuona watoto hawa wakiendelea na elimu yao kwa mafanikio makubwa. Hongereni sana walimu, wazazi, na haswa wahitimu wetu,” amesema Mhe. Ngatale.
Aidha, mgeni rasmi amesisitiza umuhimu wa maadili mema na udumishaji wa nidhamu kwa wanafunzi, akiwahimiza wahitimu wa kike kutoacha ndoto zao kwa sababu za kidunia au mahusiano yasiyo sahihi. Pia ametahadharisha kuhusu hatari za mitandao ya kijamii na matumizi mabaya ya simu za mkononi, akisisitiza kuwa vinavyoweza kuharibu ndoto za vijana.
Ahadi za Mgeni Rasmi
Nafasi muhimu katika hotuba ya Mhe. Ngatale ilikuwa ni kutoa ahadi za utekelezaji wa changamoto za shule. Miongoni mwa ahadi hizo: Kuzifikisha changamoto za uchakavu wa madarasa, ukosefu wa kiwanja cha michezo, na mashine za kurudufu mitihani kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ili kutafutiwa ufumbuzi haraka kulingana na mipango na upatikanaji wa fedha.
Amesisitiza wazazi kuendeleza sapoti kwa watoto wao wakati wote wanapokuwa majumbani wakisubiri kuanza masomo ya kidato cha kwanza au vyuo mbalimbali.
Mhe. Ngatale pia amewashauri wazazi kuendeleza maadili mema kwa watoto wao, ikiwemo kuheshimu wengine, kushirikiana katika kazi za nyumbani, na kuwa na tabia ya upendo na uadilifu, ili kujenga kizazi chenye maadili mema kwa taifa.
Sherehe hiyo imemalizika kwa mgeni rasmi kutunuku vyeti kwa wahitimu wote wa darasa la saba, huku akiwahimiza wanafunzi waliobaki kuendelea na bidii, nidhamu, utulivu, na usikivu kwa walimu wao.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ameeleza shukrani kwa mgeni rasmi na kupongeza walimu, wazazi, na wanafunzi kwa kushirikiana kufanikisha elimu bora.
Shule ya Msingi Mapinduzi “A” imeendelea kuibua watoto wenye nidhamu, maadili mema, na juhudi za kielimu zinazoweza kuwa msingi wa viongozi bora wa kesho.




















from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/XvQyxcq
No comments