Breaking News

MIRADI SABA YA BILIONI 2.4 YAZINDULIWA TANGA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AJIRA KWA VIJANA NA WATOTO


Na Hadija Bagasha Tanga, 

Changamoto ya kukithiri kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ulawiti na ajira kwa vijana Mkoani Tanga inakwenda kupatiwa ufumbuzi baada ya ujio wa miradi mikubwa saba yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 2.4.

Shirika la Botner Foundation la Nchini Uswis limetoa zaidi ya shilingi bilioni 2.4 kwajili ya ufadhili wa miradi saba ikiwemo mradi wa kukabiliana na changamoto ya ajira kwa vijana na mradi wa  malezi na makuzi ya watoto ukilenga kumaliza vitendo vya ulawiti kwenye kundi hilo

Akizunguza wakati wa uzinduzi wa miradi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Dadi Kolimba ametaka fedha zilizotolewa na wafadhili kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa kuwafikia walengwa. 

"Tunafanya uzinduzi wa miradi saba ambayo imakwenda kusaidia vijana na watoto kama mnavyofajamu nchi yetu kwa upande wa vijana kumekuwa na shida kubwa ya ajira soko la ajira katika nchi yetu ni changamoto na hivyo kupitia miradi hii ya Tanga yetu ambayo inapata ufadhili kutoka kwa Botnar foundation na wenzetu tumezindua leo miradi hii saba, "alisema Kolimba. 

"Miradi hii inakwenda kusaidia vijana katika upande wa miradi ya afya lakini pia na elimu na tumeona fedha zinazokwenda kutekeleza miradi hii  ni karibu bilioni 2.4 na sisi tutahakikisha kwamba tunasimamia vizuri miradi hii ili iweze kuwakomboa vijana katika jiji letu la Tanga waweze kujikwamua na kusimamia miradi yao na kuhakikisha wanaiendesha vizuri, "alisisitiza Kolimba. 

Mwenyekiti wa Kamati ya uendeshaji mradi wa Tanga Yetu Juma Rashid ametaka vijana kushiriki kwenye miradi hiyo ili iweze kuwanufaisha na kuleta mabadiliko kwenye maisha ya watoto na kulifanya jiji la Tanga kuwa mahali pazuri pa kuishi. 

"Awamu hii tuna miradi 7 na kati ya hii mitatu  ipo kwenye sekta ya afya na mmoja eneo la ujasiriamalli,  michezo ambayo sasa no ajira rasmi kwa vijana lakini linawaahughulisha vijana pamoja na watu wazima, "

"Eneo jingine ni la elimu , malezi na makuzi ya watoto ambapo miradi yote itakapotekelezwa vizuri na  kazi yetu kubwa kama kamati ya uendeshaji  ni kusimamia utekelezaji wa uendeshaji wa miradii hii iteekelezwevile imepangwa na itoe matokeo ambayo tunayafikiria yataleta mabadilikp katika maisha ya watoto na vijana, 

Kwa upande wake mratibu wa asasi ya kiraia ya Gift of hope Said Bandawe amesema mtadi huo utakuwa na manufaa makubwa kwa waraibu wa dawa za kulevya huku Mkurugenzi wa Taasisi ya Tayota George Bwire akisema mradi huo utasaidia kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vimekuwa vikiongezeka mara kwa mara. 

Miradi hiyo ambayo inalenga maeneo mbalimbali ikiwemo afya,  ujasiriamali,  michezo,  elimu na makuzi ya watoto ikotekelezwa ipasavyo inatarajiwa kuwa na matokeo chanya katika jiji la Tanga. 


from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/x83SYXg

No comments