DKT NCHIMBI "RAIS SAMIA NI KIELELEZO CHA USHAHIDI WA VITENDO" | AELEZA MAZURI NDANI YA ILANI YA CCM 2025-2030
Mgombea mwenza wa nafasi ya Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi amesema Dkt Samia Suluhu Hassan ni Ushahidi wa Vitendo, kwa Sababu ameelekeza nguvu katika kuhakikisha Maendeleo yanawafikia Watanzania.
Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Septemba 22, 2025 akiwa Ludewa mkoani Njombe katika muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Urais kuelekea Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 mwaka huu.
"Dkt Samia Suluhu Hassani ni Kielelezo cha Ushahidi wa Vitendo, kwa Sababu Miaka mitano iliyopita ameelekeza nguvu zake katika Utatuzi wa Changamoto mbalimbali za Wananchi, ameelekeza nguvu zake katika Kuinua huduma mbalimbali za Kijamii, ni dhahiri ameonesha kwa Vitendo kuwa kazi kubwa imefanywa na Serikali inayojali watu wake" amesema Dkt Nchimbi.
Sambamba na kauli hiyo Dkt Nchimbi ametoa ahadi kwa wana Ludewa namna Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ilivyo Jielekeza katika Utatuzi wa Changamoto hususani ya Miundombinu ya Barabara pamoja na Sekta zingine.
No comments