KADOGOSA AANZA KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA BARIADI VIJIJINI.. AAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA, MIUNDOMBINU NA UWEZESHAJI VIJANA
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa akizungumza na wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wa kampeni zake za kuwania ubunge wa jimbo hilo.
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa, akizungumza na wananchi wa Ngulyati katika mkutano wa kampeni kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi ili achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Wananchi wakiendelea kufuatilia sera za mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa katika mkutano wake wa kampeni.
Wananchi wakiendelea kufuatilia sera za mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa katika mkutano wake wa kampeni.
Wananchi wa kijiji cha Ngala wakimsikiliza mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa katika mkutano wa kampeni alioufanya kijijini hapo kwa ajili ya kunadi sera zake ili achaguliwe kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Wananchi wa Ngulyati waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kisikiliza sera za mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini Masanja Kadogosa.
****
Na Annastazia Paul, Simiyu
Mgombea ubunge wa jimbo la Bariadi vijijini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Masanja Kadogosa, ameanza rasmi kampeni zake kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi wa jimbo hilo, ili waweze kumchagua na kuwa mbunge wa jimbo hilo ambapo ameahidi kuzishughulikia na kuzitatua changamoto zinazowakabili wakulima katika uuzaji wa mazao, miudombinu ya barabara pamoja na uwezeshaji vijana katika jimbo hilo ili kuwasaidia wananchi kuwa na maisha bora, kupitia shughuli zao mbalimbali wanazozifanya.
Kadogosa ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji vya Ngala na Ngulyati vilivyopo kata ya Ngulyati jimbo la Bariadi vijijini na kueleza kuwa changamoto hizo zimekuwa kikwazo cha maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo na kwamba zitakapotatuliwa zitachochea maendeleo jimboni hapo.
"Suala la mazao, suala la kilimo ndio maisha yetu haya, kwahiyo ndugu zangu nataka mniamini, chama cha mapinduzi hakijakosea kunileta, haya tutayazungumza ya kimfumo tutayabadilisha ili kuhakikisha wakulima wananufaika na uzalishaji wao" ,amesema Kadogosa.
Aidha ameeleza namna ambavyo ilani ya CCM ya mwaka 2025 - 2030 itazishughulikia changamoto za miudombinu ya barabara katika kata ya Ngulyati.
"Tuna barabara yetu ya kutoka Bariadi - Salama inakutana na wenzetu wa Magu, kilomita 76 hiyo barabara ni muhimu sana, kazi yangu ni kufuatilia na kuhakikisha inajengwa pamoja na daraja katika mto Bariadi, na tutaimarisha ile barabara ya kutoka Gambosi kwenda Ikungulyabashashi hadi Dutwa", amesema Kadogosa
Kuhusu uwezeshaji wa vijana Kadogosa ameeleza namna ambavyo ataanzisha program zitakazowasaidia vijana kuimarisha uchumi wao.
"Vijana wanasoma si ndio? Wanamaliza shule hawana ajira, tatizo hili ni la kidunia, lakini lina majibu yake tutakuwa na miradi, pamoja na ile mikopo ambayo inatolewa kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu, lakini tutakuwa vile vile na program kwa vijana wetu ambao wanataka kufanya kazi, tutashirikiana kwa pamoja kuhakikisha kwamba vijana wetu wana kitu wanachokifanya vijijini huku huku, mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshasema katika siku 100 za uongozi wake atatoa bilioni 200 nchi nzima kwa ajili ya vijana tu na wajasiriamali, mimi kazi yangu ni kuibua miradi kwa vijana wenzangu" ,amesema Kadogosa.
Kadogosa ataendela na kampeni kwa ajili ya kuomba ridhaa kwa wananchi wa jimbo la Bariadi vijijini ili wamchague na kuwa mbunge wa jimbo hilo.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/Yq4zuXy
No comments