DKT. JUDITH AWAOMBA WATANZANIA KUENZI AMANI
Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwanamke na Nguvu ya Kijani, Dkt. Judith Mhina Spendi, ametoa wito kwa Watanzania wote kusimama pamoja kulinda amani ya taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dkt. Judith alitangaza kongamano la amani litakalofanyika kuanzia Oktoba 25 hadi 27, 2025 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama, likiwakutanisha viongozi wa dini, vijana, wafanyabiashara, na taasisi mbalimbali zenye malengo ya kuhamasisha amani na mshikamano wa kitaifa.
Dkt. Judith alisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo, akieleza kuwa Tanzania imeendelea kupiga hatua kubwa kiuchumi kutokana na utulivu wa kisiasa na kijamii uliopo.
“Hakuna maendeleo bila amani, hakuna uchaguzi huru bila utulivu, na hakuna taifa imara bila mshikamano,” alisema Dkt. Judith.
Aidha, alitoa rai kwa Watanzania wote kuwa sauti ya amani, umoja na ukweli, akihitimisha hotuba yake kwa ujumbe wenye mguso wa kipekee kwa taifa:
Kongamano hilo linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kuimarisha ari ya amani na utulivu kabla, wakati, na baada ya uchaguzi, huku likiwakutanisha wadau mbalimbali wanaojali mustakabali wa taifa.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/INulisR




No comments