NSSF YAANZA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA JIJINI ARUSHA
Na Bora Fadhili - Arusha
Aidha, Meneja wa Huduma kwa Wateja, Robert Cosmas Kadege, amesema kampeni hii ina umuhimu mkubwa kwa sababu inahamasisha wanachama kuchangia kwa hiari. Kadege alibainisha kuwa mwanachama anaweza kuchangia kwa hiari kupitia njia mbalimbali za kidigitali, na hata wale wasio na simu janja wanaweza kuchangia kwa kutumia menu husika kwenye simu zao za kawaida.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Taifa Masha Mshomba, amesisitiza kuwa wiki hii ya huduma kwa wateja inalenga kuonyesha huduma bora kwa wateja na kuwashukuru watumishi kwa jitihada zao katika utoaji wa huduma hizo. "Bila wateja hatuwezi kuwa na mfuko," alisema.
Masha Mshomba pia aliongeza kuwa huduma kwa mfumo wa TEAMA imefikia asilimia 97 na wanatarajia kufikia asilimia 100 kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kuhusu changamoto za wateja ambao bado hawajafikiwa, alihakikishia kuwa wataendelea kuwafikia na kuwapatia huduma bora zaidi.
Aidha, alisema kuwa thamani ya mfuko kwa mwaka 2024/2025 imefikia trilioni 9.9, ikionyesha ukuaji mkubwa ikilinganishwa na thamani ya trilioni 4.8 mwezi Machi 2021, ongezeko la zaidi ya asilimia 100. Alimshukuru wafanyakazi wa NSSF kwa ushirikiano wao katika kufanikisha mafanikio haya.
Aidha Kuhusu michango ya hiari, Masha Mshomba amesema kuwa kwa wale wasioajiriwa serikalini au sekta binafsi, wanaweza kuchangia kwa hiari kila wiki, mwezi au hadi miezi 12 mfululizo bila kupata adhabu yoyote (penaty).
Aliongeza kuwa NSSF ni muhimu kwa sababu husaidia wafanyakazi wakati wa matatizo kama vifo au ugonjwa, ambapo familia na wagonjwa hawatahangaika kutafuta misaada ya kifedha.
Mmoja wa wastaafu aliyeongea katika maadhimisho hayo alisema kuwa pensheni zao huliwa kwa wakati na hawajawahi kukosa malipo, na kwamba wastaafu wamejaliwa sana. Aliwahi kusisitiza umuhimu wa NSSF kwa wafanyakazi wanaoendelea kufanya kazi.
Aidha, Jackiline Emmanuel, aliyepokea mafao ya uzazi, aliipongeza NSSF kwa huduma nzuri alizopata na kusema amefurahia kuwa na mfuko huu unaowajali wanachama wake.
Lightness Emmanuel Munga pia alieleza jinsi NSSF ilivyomsaidia kwa malipo ya wake upo wake wa matibabu baada ya kupata tatizo la mgongo na kuenda India kwa matibabu zaidi, na sasa anaendelea kupata huduma kupitia mfuko huo.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/NItLzXu
No comments