MC PILIPILI AMEUAWA KWA KIPIGO
Kaka wa marehemu Emmanuel Mathias, maarufu kama MC Pilipili, Christopher Matebe amesema matokeo ya uchunguzi wa awali yameonyesha kwamba kifo cha mdogo wake kilisababishwa na kupigwa na watu wasiojulikana hii ni baada ya Mwili wake kukutwa na majeraha
Kaka wa MC Pilipili ameyasema hayo Novemba 18,2025 wakati akitoa Mrejesho wa awali juu ya Uchunguzi unao endelea ambapo ameushukuru uongozi wa Hospitali ya General pamoja na Mbunge wa Dodoma Mjini Antony Mavunde kwa kuwa karibu na familia katika kipindi hiki kigumu.
Amesema kuwa shughuli za kumuaga zinaendelea nyumbani kwao na ibada ya maziko itafanyika nyumbani kwao Swaswa Dodoma na amesisitiza taratibu za Uchunguzi ameiziachia Mamlaka za Serikali.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/stScBrM
No comments