Bodi ya Mikopo yawazawadia waajiri 12
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini (HESLB) imetoa zawadi maalum waajiri 12 wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, kutokana na kuwasilisha kwa wakati makato ya wafanyakazi wao waliokopeshwa.
Mkurugenzi mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru, alisema waajiri hao, wamekuwa mfano kwani wamekuwa wakikata kwa wakati fedha za wafanyakazi wao kiasi cha asilimia 15 katika mshahara na kuwasilisha kulingana na sheria na taratibu.
Aliwataja waajiri hao kwa mkoa wa Arusha ni Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), World Vision Tanzania, Vision Fund Tanzania, The School of St Jude, Off- Grid Electric Company (Zola) na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Arusha(AUWSA).
Kwa mkoa wa Kilimanjaro ni Bonite Bottlers Limited, Marenga Investment, Uchumi Commercial Bank, Tanganyika Planting Company Ltd (TPC) Mwenge Catholic University na Kilimanjaro Airport Development Company (Kadco).
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo aliwapongeza waajiri hao kwa kutimiza wajibu wao vizuri na kuwataka waajiri wengine nchini kuiga mfano, ili kuwezesha bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuendelea kutoa huduma hiyo.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2ECclWN
No comments