Breaking News

Indonesia yazidi kukumbwa na matetemeko ya ardhi

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.3 limetokea katika jimbo la Gorontalo kwenye kisiwa cha Sulawesi nchini Indonesia.

Mamlaka ya hali ya hewa nchini humo (BMKG),yametangaza kuwa tetemeko hilo limefikia kina cha kilomita 21.

Hakunaripoti iliyotolewa kuhusu mtu kupoteza maisha au uharibifu wa mali kutokana na tetemeko hilo la ardhi.

Mnamo 28 Septemba 2018,tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.5 lilitokea katika kisiwa cha Sulawesi na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 4000 huku wengine wengi wakiwa wamejeruhiwa.

Indonesia imekuwa ikiandamwa na matetemeko ya ardhi ya hapa na pale na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2GO8w36

No comments