Breaking News

Kesi ya Zitto dhidi ya Spika Ndugai yapingwa kalenda


Kesi ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika wa Spika wa Bunge, Job Ndugai ya kuhoji mamlaka ya Bunge kumuhoji CAG imeahirishwa hadi Machi 26 mwaka huu.

Kesi hiyo ya Kikatiba namba 01/2019 ilifunguliwa Mahakama Kuu, Masjala Kuu na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe dhidi ya Spika.

Zitto Kabwe aliiomba mahakama itoe tafsiri ya kinga ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyopo kikatiba na tafsiri ya sheria ya haki, kinga na madaraka ya Bunge katika kushtaki wanaodaiwa kulidhalilisha Bunge.

No comments