Hatimaye TFF watoa tamko kuhusu mchezaji wa Yanga SC, Abdallah Shaibu 'Ninja'
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeridhia ombi la Yanga SC la kuahirisha kusikiliza shauri dhidi ya Abdallah Shaibu kwa vile wakati anapata mwito wa kuhudhuria alikuwa mkoani.
Sasa shauri dhidi yake litasikilizwa katika kikao kijacho, na Kamati haitapokea udhuru wowote isipokuwa kama atakuwa na majukumu katika timu ya Taifa.
Awali kulizuka taarifa kuwa TFF kupitia Bodi ya Ligi wamemfungia Ninja michezo mitatu kwa kitendo cha kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Coastal Union katika mechi ambayo ilimalizika kwa timu hizo kwenda sare ya mabao 1-1 huko Mkwakwani, Tanga, kitu ambacho kinaonekana si kweli.
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2S3Zn7y
No comments