Breaking News

Matola aahidi ushindi kesho dhidi ya Simba

Klau ya Lipuli kesho itashuka dimbani kukipiga na klabu ya Simba kwenye kwenye Uwanja wa Samora huku rekodi zikionyesha kwamba tangu msimu wa 2017/2018 Lipuli ilipopanda daraja, hakuna hata timu iliyoonja ushindi kwa mwenzake.

Kocha wa Lipuli Selemani Matola amesema atawafunga Simba licha ya timu hiyo kuwa na matokeo mazuri katika mechi za hivi karibuni.

Matola alisema amewatazama wapinzani wake kwa ukaribu na kujua udhaifu wao, hali ambayo imemfanya aamini kwamba kesho atavunja rekodi iliyowekwa kwa timu hizi mbili.

“Siyo mechi rahisi, tumejipanga kamiligado, mechi tatu zimepita hakuna aliyebeba pointi tatu kwa mwenzie, sasa sisi tuna hamu sana kuwa wa kwanza kubeba pointi tatu nyumbani.

“Najua Simba ni timu nzuri na ina kitu cha kipekee kwa sasa kutokana na ushindi ambao wamepata hivi karibuni, lakini hilo halitupi taabu kwa kuwa bado ni Simba walewale ingawa wana kitu kipya walichonacho, tutawazuia nyumbani na kuvunja rekodi ile ya michezo yetu mitatu tuliyocheza nao,” alisema Matola.

Katika michezo hiyo mitatu ambayo walicheza nao msimu wa 2017/18 wakiwa nyumbani Simba walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 kwenye Uwanja wa Samora, mchezo wa marudiano Lipuli walilazimisha sare ya bao 1-1 Uwanja wa Taifa.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza msimu huu, zilitoka suluhu Uwanja wa Taifa.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2IBRPJX

No comments