Mwanamke apasuliwa uso na mumewe kwa kukataa penzi kinyume na maumbile
Imeripotiwa kuwa mwanamke mmoja mkazi wa Kijichi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, mumewe amempiga na kumjeruhi baada ya kumkatalia kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Mwanamke huyo amedai kuwa mume wake amekuwa akimtaka wafanye mapenzi kinyume na maumbile muda mrefu lakini amekuwa akikataa, kwani ni dhambi kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya kiislamu.
Pia amesema kwa muda mrefu ndoa yake imeingia kwenye mgogoro na mumewe amekuwa akimwambia kuwa hajui mapenzi.
“Alianza kunitaka kinyume na maumbile miezi mitatu tangu anioe nikamkatalia, mpaka nikapata mimba ikiwa na miezi saba bado akawa anataka nikamkatalia,” amesema mwanamke huyo.
Mwanamke huyo amesema Majirani zake wanaomfahamu mwanamme huyo, walimweleza kuwa tabia hiyo ameizoea na ndiyo imesababisha kuachana na wake zaidi ya wawili.
Kwa upande mwingine, mwanaume huyo amekanusha tuhuma hizo na kueleza kuwa mgogoro wa ndoa yake umesababishwa na wakwe zake kumdai mahari na kumsimanga kuwa ni maskini.
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2X74XKn
No comments