Breaking News

Syria yajadiliwa na Urusi, Uturuki na Iran


Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemueleza mwenzake wa Urusi Vladimir Putin kwamba watahitaji msaada wa Urusi kufuatia uamuzi wa Marekani wa kuyaondoa majeshi yake nchini Syria.

Erdogan na Putin wamekutana hii jana mjini Sochi kuijadili Syria. Awali, Erdogan alikiri kuwepo kwa hali ya sintofahamu kufuatia uamuzi huo wa Marekani.

Akizungumza akiwa mjini Sochi nchini Urusi, Erdogan amesema ni muhimu kwao kushirikiana katika kukabiliana na changamoto hiyo mpya. Amesema hayo katika hotuba yake iliyorushwa kwenye televisheni wakati wa mkutano wa kilele baina ya Urusi, Uturuki na Iran uliolenga kujadili mustakabali wa mzozo wa Syria. Rais wa Iran, Hassan Rouhani pia amehudhuria.

Uturuki imeiomba Urusi kushirikiana na vikosi vyake vilivyopo kwenye kambi ya jeshi la anga la Urusi ya Khmeimim iliyoko magharibi mwa Syria. Uturuki inataka kuweka ukanda salama karibu na mpaka wake ili kuondosha wasiwasi wa kiusalama.




from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2S0ZfWs

No comments