Breaking News

Rais aliekuwa madarakani nchini Senegal ashinda katika uchaguzi

Rais  aliekuwa madarakani  nchini Seengal Macky Sall ameshinda katika uchaguzi mkuu ulioanyika nchini humo kama inavyoonesha matokeo ya  kwanza ya uchaguzi huo.

Macky Sall amegombea kiti cha urais  katika uchaguzi huo  kupitia tikiti ya chama tawala.

Vyama vya upinzani nchini humo vimetoa msiamamo tofauti vikifahamisha kuwa huenda vikakata rufaa  na kupinga matokeo ya  uchaguzi.

Macky Sall ameshinda  kiti cha urais katika  mzunguko wa kwanza. Zoezi la upigaji kura lilianza mapema Jumapili na kumaliza majira ya jiano ambapo  vituo vya mwisho vya kupiga kura vilifungwa usiku saa tatu majira ya Senegal.

Idrissa Seck, mmoja miongoni mwa wagombea wa upinzani aliwasili katika ngome yake ya mjini Thiès, akishirikiana na Ousmane Sonko, mgombea mwengine wa upinzani anayewania kiti cha urais.

Bila kutaja kura alizopata, kiongozi huyo wa chama ch Rewmi alitoa wito kwa wafuasi wake kujiandaa kwa duru ya pili ya uchaguzi kwa utulivu huku akishtumu chama tawala  na mgombea wake Macky Sall wizi wa  kura.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2U8eC1j

No comments