Breaking News

Rais Kim na Trump waanza siku ya pili ya mazungumzo


Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wameanza siku ya pili ya mazungumzo, baada ya kukutana jana katika hafla ya chakula cha jioni.

Trump alipokutana na Kim katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi hapo jana na akasema kuwa ameridhishwa na kasi ya mazungumzo, licha ya kuwepo kwa ukosoaji kuwa hayasongi haraka iwezekanavyo.

Ikulu ya Marekani imesema viongozi hao wawili wanapanga kusaini "makubaliano ya pamoja” baada ya kufanya mazungumzo zaidi leo, Hata hivyo hawajatoa maelezo yoyote kuhusu sherehe hiyo ya utiaji saini, ijapokuwa mazungumzo ya pande zote yamejumuisha uwezekano wa taarifa ya kisiasa ya kutangaza kumalizika kwa Vita Vya Korea vya mwaka wa 1950 – 53, ambayo baadhi ya wakosoaji wanasema bado mapema.

Maafisa wa Marekani na Korea Kaskazini wamesema Trump na Kim pia walijadili hatua za kuondoa silaha za nyuklia, kama vile kuwaruhusu wakaguzi kushuhudia kuharibiwa kwa kinu cha nyuklia cha Korea Kaskazini cha Yongbyon.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Vra9GX

No comments