Breaking News

Watu 20 wafariki dunia katika ajali ya Treni


Watu 20 wamefariki dunia na wengine 40 kujeruhiwa baada ya kutokea ajali ya treni katika njia kuu ya treni nchini Misri.

Tukio hilo limetokea baada ya treni hiyo kugonga kizuizi cha kupunguza kasi, katika kituo kimoja cha treni katikati ya mji, na ajali hiyo imesababishwa na kulipuka kwa tanki la mafuta la treni hiyo, hali iliyosababisha Majengo ya jirani pia kuungua.


Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, lakini saa chache baadaye Waziri anayeshughulika na usafiri Hisham Arafat alijiuzulu.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Ahmed Mahmoud ameliambia shirika la Habari la AFP, kuwa alitoa miili ya Watu 20 na kuiweka kwenye gari la wagonjwa ikiwa yote imeungua na moto.

Aidha amesema kawaida ya treni ikikaribia Kituoni huja kwa mwendo wa taratibu lakini treni hiyo ilikuwa katika mwendo wa kasi.




from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2EBG7uO

No comments