Breaking News

RC Makonda aweka wazi njia tatu za kuifikisha Taifa Stars AFCON


Mwenyekiti wa Kamati ya Saidia Taifa Stars Ishinde Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekutana na wajumbe wa Kamati hiyo katika Kikao cha Kwanza kilichofanyika kwenye Hoteli ya Serena,Dar es salaam ambapo amewaomba wananchi kuwa kitu kimoja katika kuisapoti timu hiyo.

RC Makonda amesema majukumu makubwa matatu watakayoanza nayo Kama kamati ni Kuirudisha timu kwa wananchi, kuweka maandalizi mazuri ya timu na uwezeshaji wa timu.
Aidha RC Makonda amesema katika kikao cha kamati imepanga kukutana na watu wa makundi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Dini, Wasanii, Wanasiasa, Wamiliki wa Vyombo vya Habari na wadau mbalimbali ili kwa pamoja tuiunge mkono timu ya Taifa.

Kamati hiyo inaongozwa na RC Makonda ambaye ni Mwenyekiti, Katibu wake akiwa ni Mhandisi Hersi Said ambapo Wajumbe wa kamati hiyo ni Mohamed Dewji, Haji Manara, Jerry Muro, Farouk Barhoza, Salim Abdallah, Mohamed Nassor, Patrick Kahemele, Abdallah Bin Kleb, Tedy Mapunda, Philimon Ntaihaja, Farid Nahid na Faraji Asas.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2BTi3ln

No comments