Wauza Vipodozi wapewa onyo na TFDA
Wafanyabiashara wa Vipodozi wanaoendelea kukiuka sheria za dawa na vipodozi kwa kuuza vitu vilivyopigwa marufuku wameonywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Kati.
Meneja wa Mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Dk. Englibert Bilashoboka alisema TFDA inaendelea na misako ya kuwatafuta wanaokiuka sheria ili wachukuliwe hatua.
"Licha ya kutoa elimu kwa wananchi kuepukana na vipodozi vinavyokuwa na madhara, baadhi ya watumiaji wa vipodozi kama hivyo ndio wamekuwa na ushawishaji kwa wafanyabiashara kuingiza vipodozi vilivyopigwa marufuku,” alisema Bilashoboka
Aidha, alisema kuwa pamoja na juhudi ya kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara hayo, bado vinauzwa kwa siri kwenye baadhi ya maduka ya vipodozi.
Meneja huyo alisema kwa sasa wanashirikiana na raia wema kusaka vipodozi hivyo na imeweka mfumo wa ufuatiliaji wa bidhaa katika masoko.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2U62ptO

No comments