Breaking News

Utoaji leseni migodi mikubwa wakamilika


Serikali kupitia Wizara ya Madini inakamilisha taratibu za utoaji wa leseni kwa Migodi mikubwa ambazo hazijawahi kutolewa nchini, huku migodi hiyo ikitarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.

Hayo yalibainishwa juzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila, alipokutana na viongozi wa jumuiya ya watendaji wakuu wa taasisi binafsi ofisini kwake, jijini Dodoma.

Viongozi hao walikutana na Prof. Msanjila kwa lengo la kujitambulisha, kuelewa shughuli za serikali upande wa sekta ya madini, kupata uelewa kuhusu mabadiliko ya Sheria ya Madini na namna pande hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kuendeleza sekta husika.

Prof. Msanjila aliwakaribisha viongozi hao kwenye sekta ya madini, huku akiwataka kuzishawishi kampuni mbalimbali kuwekeza nchini hususani katika shughuli za uongezaji thamani madini na kueleza kuwa suala hilo ni miongoni mwa maeneo ambayo serikali inayapa kipaumbele ikiwamo ujenzi wa vinu vya kusafisha na kuyeyusha madini.

Kuhusu Sheria ya Madini ya Mwaka 2017, Prof. Msanjila alisema hakuna tatizo lolote katika utekelezaji wa sheria na kueleza kuwa serikali kupitia Wizara ya Madini inapokea wawekezaji wengi wenye utayari na nia ya kuwekeza nchini, huku utekelezaji wa sheria hiyo ukiwa si kikwazo.






from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Vo9nKX

No comments