Kocha wa Mbeya City awajia juu mashabiki
Kocha Mkuu wa Mbeya City, Nsanzurwimo Ramadhan amewachana mashabiki wa timu yake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara jana
Hatua hiyo imekuja kutokana na matokeo ya hivi karibuni ambayo yamekuwa hayawafurahishi hivyo kufikia hatua ya kutupiwa lawama na kulitukana benchi la ufundi.
Kocha huyo amesema mashabiki wa timu yao wamekuwa hawana uchungu na kutoonesha uzalendo wa kuishabikia timu hiyo inapofanya vibaya kitu ambacho kimesababisha mpaka waanze kutukana.
Ramadhani amezungumzia suala hilo kuwa kero huku akifunguka kuwa timu inapofanya vibaya si kwamba iache kuungwa mkono bali juhudi za hamasa ziendelee.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Nzhamm
No comments