Wabunge 17 wa upinzani wasota Mahakamani
Wabunge 17 wa upinzani nchini wanakabiliwa na kesi katika mahakama mbalimbali nchini, ambapo wanne kati yao (Freeman Mbowe, Esther Matiko, Peter Lijualikali na Susan Kiwanga) wapo mahabusu.
Pia Wawili kati ya hao 17 (Peter Lijualikali, Joseph Mbilinyi) walishawahi kutumia kifungo jela.
Miongoni mwa kesi inayofuatiliwa na wengi ni ile inayowakabili baadhi ya Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
viongozi hao ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika, mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya, na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk Vincent Mashinji na mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa.
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16 mwaka jana Dar es Salaam.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2GMltui
No comments