Trump na Kim kuanza mkutano wa pili wa kilele Vietnam
Rais Donald Trump wa Marekani na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jogn Un wanaanza mkutano wao wa pili wa kilele chini ya mwaka mmoja katika mji mkuu wa Vietnam Hanoi.
Ikulu ya Marekani imesema Trump atakutana na Kim katika hoteli ya kihafari mjini Hanaoi ya Metropole iliyojengwa wakati wa enzi ya ukoloni wa Wafaransa na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana kwa dakika 20 kabla ya kushiriki hafla ya chakula cha jioni itakayodumu kwa saa moja na nusu.
Rais Trump aliwasili Jana Mjini Hanoi na ndege ya Air Force One, na akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Nimewasili Vietnam. Ahsanteni sana watu wote kwa makaribisho mjini Hanoi. Umati wa ajabu na upendo mkubwa”.
Rais Kim aliwasili kwa kutumia treni mapema jana, baada ya safari ya siku tatu ambayo ilikuwa ya umbali wa kilomita 3,000 kutoka mji mkuu wa Korea Kaskazini; Pyongyang, kupitia China. Alitumia sehemu ya mwisho ya safari yake kutoka mpaka wa Vietnam hadi Hanoi kwa kutumia gari.
Viongozi hao wawili, ambao walionekana kuanzisha mahusiano mazuri na ya kushangaza katika mkutano wao wa kwanza wa kilele nchini Singapore Juni mwaka jana, wataandamana katika hafla ya chakula cha jioni na wasaidizi wawili na wakalimani, kabla ya kukutana tena kesho ALhamisi.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2NA6R1G
No comments