Breaking News

Halmashauri zaombwa kujifunza ujenzi wa soko la Njombe


 Na Amiri kilagalila-Njombe

Halmashauri zingine Nchini  zimeombwa kujifunza namna ujenzi wa mradi wa soko kuu la Njombe unavyojengwa ili kuendana na ujenzi wa majengo yenye viwango.

Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa Tamisemi mh.Joseph Sinkanda Kandege wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa soko kuu la Njombe Mjini.

 “Miongono mwa masoko ambayo  yanajengwa kwa ustadi mkubwa ni pamoja na hili soko la Njombe TC kwanza nawapongeza kwa kuchagua mradi huu na uhakika mradi ukikamilika  kwa kiwango wanachotarajia itakuwa ni miongoni mwa Miradi mizuri kabisa,halmashauri Zingine waje kujifunza katika mradi huu".

 “Ramani hii nimeridhika nayo ni ramani ya kisasa soko likikamilika litakuwa ni miongoni mwa masoko ya kisasa katika  halmashauri zetu,nampongeza mkurugenzi na timu yake,wilaya na mkoa  na sisi kama serikali miradi kama hii tutatoa sapoti ili ikamilike kwa wakati na wananchi waanze kunufaika nayo”alisema Kandege

 Soko hilo linaloghalimu zaidi ya bilioni saba linategemewa kukamilika mwezi wa sita na kuanza kuwanufaisha zaidi ya wafanyabiashara 1000 mjini Njombe.


from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2L8mYpC

No comments