HAO MASHABIKI WA SIMBA NA BIASHARA UNITED MARA KAMA WOOOTE
KUELEKEA kwenye mchezo wa leo wa ligi kuu kati ya Biashara United na Simba utakaochezwa uwanja wa Karume majira ya saa 10:00, mashabiki wamejitokeza kwa wingi kuujaza uwanja huo.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mashabiki wamejitokeza wengi kabla ya saa tano kamili tayari Uwanja ulikuwa umejaa.
"Kabla ya saa tano kamili mashabiki walikuwa wamejitokeza wengi sana na wameujaza uwanja wa Karume nje na ndani hii ndio Simba," amesema.
Kocha wa Biashara United, Amri Said amesema kuwa uwepo wa mashabiki utaongeza morali kwa wachezaji wake kupambana kupata matokeo chanya.
"Uwepo wa mashabiki ni kitu cha kujivunia kwetu hivyo tuna imani tutafanya kila juhudi kupata pointi tatu," amesema
from SALEH JEMBE


No comments