Japani kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo nchini
Serikali ya Japani imesema itaendelea kuisaidia Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Maendeleo hususani miradi ya kijamii na watoto, ili kuhakikisha nchi inakuwa na watu wanaoweza kuiletea maendeleo.
Kauli hiyo imetolewa mapema ya leo na Balozi wa Japani nchini Ndufu Shinichi Goto, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi walipotembelea kituo cha kulea watoto cha Amani kilichopo mkoani Iringa ambacho Serikali ya Japan imesaidia ujenzi wa mabweni kwa ajili ya watoto kituoani hapo.
Pamoja na mambo mengi Balozi Goto amekagua shughuli za kilimo cha mbogamboga zinazoendeshwa na kituo hicho.
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2ZChgPJ

No comments