Breaking News

Leo hatujacheza mchezo mzuri - Kocha Mkuu wa Simba SC


Kocha Mkuu wa Simba SC, Patrick Aussems amefunguka mara baada ya kuwalaza  KMC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) kwa goli 2-1.

Patrick Aussems amesema licha ya kupata ushindi huo mwembamba kikosi chake hakijacheza mchezo mzuri kwa siku ya leo.

“Leo hatujacheza mchezo mzuri, kiwango hakikuwa tulichokitegemea, lakini hilo linatokea kwenye mpira, hatimaye tumepata tulichokuwa tukitafuta”- Kocha Patrick Aussems baada ya mchezo wa leo dhidi ya KMC FC

Mchezo huo uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, wafungaji wa leo kwa upande wa Simba SC ni Emmanuel Okwi na John Bocco, huku kwa upande wa KMC ni Hassan Kabunda.



from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2UGHexQ

No comments