Breaking News

Waalimu Morocco waandamana kisa mikataba ya ajira, Polisi waingilia kati


Zaidi ya waandamanaji 70 wamejeruhiwa baada ya polisi katika mji mkuu wa Morocco wa Rabat, wakitumia maji yanayotoka kwa kasi kutawanya mkusanyiko wa maelfu ya walimu waliokuwa wakiandamana wakilalamika dhidi ya kanuni za mikataba yao ya kuajiriwa.

Walimu waliopaaza sauti zenye ujumbe wa kutaka haki ya kijamii, na kupinga uongozi mbovu katika shule za uma, walijaribu kupiga kambi nje ya bunge la taifa, katikati mwa Rabat, wakitaka matakwa yao kushughulikiwa, lakini polisi walitumia nguvu kuvunja maandamano hayo.

Zaidi ya walimu 55,000 walioajiriwa kwa kandarasi za muda mwaka 2016, walianzisha mgomo mwezi Machi mwaka 2019 na kufanya maandamano makubwa ili kuhimiza matakwa yao yatekelezwe ya kuajiriwa kwa mikataba ya kudumu ili kuboresha hali yao hasa watakapostaafu.

Walimu wanaofanya kazi kwa mkataba wa mda mfupi nchini Morocco wanalipwa dola 520, sawa na wenzao walioajiriwa kwa mkataba wa kudumu, lakini hawapokei marupurupu yoyote, ikiwemo malipo ya pensheni.

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2VsMcCR

No comments