Mexico: Watu 19 wauawa katika makabiliano ya magenge
Watu 19 wameuawa katika makabiliano kati ya magenge mawili ya uhalifu katika jimbo la kaskazini magharibi mwa Mexico la Chihuahua.
Taarifa ya ofisi ya mwendesha mashitaka jimbo la Chihuahua imesema vikosi vya usalama vilipelekwa katika mji wa Madera haraka baada ya kufahamishwa kuhusu mapambano hayo Ijumaa jioni.
Miili ya raia 18, magari mawili, maguruneti mawili bunduki 18 vilipatikana katika eneo la tukio. Watu wawili waliuokuwa wamejeruhiwa pia walipatikana na kupelekwa hospitali.
Mmoja alifariki dunia baadaye hospitalini wakati mwingine akawekwa kizuizini.
Mexico imekuwa ikishuhudia kiwango kikubwa cha machafuko kwa miaka mingi, kutokana na magenge yanayohusika na ulanguzi wa dawa za kulevya, utekaji nyara na unyang'anyi.
Kulikuwa na visa 2,585 vya mauaji mwezi Machi licha ya hatua ya kuwataka watu kuepuka mikusanyiko katika juhudi za kupunguza kusambaa kwa janga la virusi vya corona.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2JHCHIu

No comments