Breaking News

Wafungwa waambukizwa virusi vya corona Pakistan


Maafisa nchini Pakistan wanasema wafungwa kadhaa katika jela moja nchini humo wameambukizwa virusi vya corona. Zaidi ya wafungwa wengine 150 wanadaiwa kuambukizwa huku visa vya maambukizi nchini humo vikiendelea kuongezeka katika taifa hilo maskini.

Ripoti zinaarifu kuwa karibu wafungwa 49 katika gereza lililoko mjini Lahore mashariki mwa nchi hiyo wamepimwa na kupatikana na virusi hivyo.

Mripuko huo unadaiwa kuanza kutoka kwa mfungwa mmoja aliyekamatwa kwa ulanguzi wa dawa za kulevya na alikuwa amerudi nchini humo kutoka Italia mwezi uliopita.

Alipatikana kuwa na virusi hivyo Machi 23. Afisa wa uhusiano mwema katika gereza hilo Amir Rauf Khawaja amesema maafisa wa afya wanazuru kila siku na wameweka eneo la kuwatenga wafungwa watakaopatikana na virusi hivyo.


from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2y19gOV

No comments