Breaking News

Malkia Elizabeth amtakia Waziri Mkuu Johnson afueni ya haraka


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson yuko imara katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kupewa oksijeni kwa ajili ya kumsaidia kupumua wakati anapopambana na maradhi ya covid-19.

 Ofisi yake lakini imesema hajawekewa mashini za kusaidia kupumua. Haya yanajiri wakati ambapo waziri wake wa mambo ya nje anaongoza juhudi za nchi hiyo za kupambana na virusi vya corona.

 Johnson alilazwa hospitali Jumapili baada ya kuendelea kuonyesha dalili za virusi vya corona siku kumi baada ya kupimwa na kupatikana na virusi hivyo.

Malkia Elizabeth wa pili kupitia ujumbe uliotolewa na kasri la Buckingham amemtakia Johnson afueni ya haraka na pia akatuma ujumbe kwa mchumba wake na familia yake.

Mchumba wake Johnson, Carrie Symmonds, ambaye ni mja mzito alipatikana na virusi vya corona pia.


from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/34kEWeh

No comments