Breaking News

BARAZA LA HABARI KENYA LAVUTIWA NA MAIPAC, LAAHIDI KUSHIRIKIANA KUTOA MAFUNZO KWA WANAHABARI


Mkurugenzi mtendaji MAIPAC,Mussa Juma akimkabidhi Mkurugenzi wa mafunzo na Maendeleo wa baraza la habari Kenya Victor Bwire kitabu cha maarifa ya asili katika uhifadhi wa mazingira kilichoandaliwa na MAIPAC ambacho kinasambazwa bure
Mwandishi wetu,maipac

Baraza la Habari la Kenya(KMC),limetembelea Ofisi za Taasisi ya wanahabari ya usaidizi wa jamii za pembezoni(MAIPAC) jijini Arusha na kuvutiwa na kazi za Taasisi hiyo na kuahidi kushirikiana kuwajengea uwezo wanahabari juu ya masuala ya mabadiliko ya tabia nchi na Matumizi sahihi ya akili mnemba(AI).

Mkurugenzi wa Mafunzo na Maendeleo wa baraza hilo,Victor Bwire akizumgumza na watendaji wa MAIPAC baada ya kupata taarifa za utendaji wa shirika hilo,licha ya kupongeza ameahidi baraza hilo kushirikiana na MAIPAC kuwajengea uwezo wanahabari.

"Kuna waandishi wa habari wa Kenya pia wanafanyakazi na hizi jamii za pembezoni hivyo tutawaunganisha na wanachama wa MAIPAC kupata mafunzo zaidi ya juu ya mabadiliko ya tabia nchi na masuala ya AI kwa sababu mazingira yanafanana",amesema.

Bwire amesema, jamii za pembezoni za Tanzania na Kenya zinaendelea kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kwa wanahabari ni muhimu kusaidia jamii hizo kuwapa elimu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi lakini pia kuweza kuhimili mabadiliko hayo.

"Nawapongeza sana MAIPAC kwa miradi yenu ,nyie kama wanahabari mnafanyakazi nzuri sana katika jamii hizi katika miradi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi,miradi ya kurekodi maarifa ya asili lakini pia miradi ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto",amesema.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa MAIPAC Mussa Juma amesema taasisi ya MAIPAC inaundwa na waandishi wa habari kutoka mikoa mbalimbali Tanzania ambao wamekuwa wakiandika masuala ya mazingira na katika jamii za pembezoni.

Juma amesema , MAIPAC imekuwa na miradi kadhaa ikiwepo kurekodi maarifa ya asili kwa jamii za pembezoni katika uhifadhi wa mazingira,misitu na vyanzo vya maji.

"Lakini pia tumekuwa na mradi wa kusaidia jamii kutunza vyanzo vya maji,mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto",amesema

Amesema miradi hiyo,inafadhiliwa na taasisi kadhaa ikiwepo mfuko wa mazingira duniani(GEF) kupitia programu ya miradi midogo ambayo inaratibiwa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) Tanzania na ofisi ya makamu wa Rais Mazingira na shirika la kimataifa la Cultural Survival.

Hata hivyo amesema kwa wanahabari wanachama wa MAIPAC wanahitaji sana mafunzo juu ya masuala mabadiliko ya tabia nchi,masuala ya akili mnemba na masuala ya biashara ya hewa ya ukaa na taratibu zake.

Katika ziara hiyo, Bwire ameambatana na viongozi wengine wa MAIPAC, Stella Kaaria Meneja wa utafutaji fedha na mahusiano,Careen Mang'eni na Evaes Teddy.


from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/FOe68uk

No comments