WAKUU WA TAASISI ZA HABARI WASHUHUDIA UWASILISHAJI BAJETI YA HABARI

Wakuu wa Taasisi za Kihabari nchini kwenye picha ya Pamoja na Waziri wa Habari Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Paramagamba Kabudi, Naibu Waziri Hamis Mwinjuma na Katibu Mkuu na Msemaji Mkuu wa Serikali Greson Msigwa baada ya uwasilishwaji wa bajeti ya Wizara ya habari, utamaduni, Sanaa na Michezo Bungeni Leo Jijini Dodoma.
Wakuu hao ni pamoja na Katibu wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Misa Tanzania {Misa Tz), Edwin Soko, Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Wafanyakazi Waandishi wa Habari Nchini (Jowuta) na Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Jukwaa la Wahariri TEF, Caren-Tausi Mbowe pamoja na Mhariri Mkuu mstaafu wa Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/XWwJhGK
No comments