Breaking News

FADHILI SALMON NAFUTARI ACHUKUA FOMU YA UBUNGE JIMBO LA ITWANGI, SHINYANGA VIJIJINI


Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog.

Fadhili Salmon Nafutari, Mtanzania mzalendo na kijana mwenye maono ya kweli ya maendeleo, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Itwangi, Wilaya ya Shinyanga. akiwa na msukumo wa kulijenga jimbo hilo kupitia rasilimali zake za asili na nguvu kazi ya wananchi wake, Fadhili anakuja na dira mpya ya maendeleo yenye kugusa maisha ya kila mwananchi.

Fadhili Salmon Nafutari amechukua fomu mapema leo Juni 30, 2025 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini. 

Kwa miaka kadhaa, Fadhili amekuwa mstari wa mbele katika masuala ya maendeleo ya wananchi, akiwa amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi zikiwemo:

· Kiongozi wa Chama cha Wachimbaji Wadogo – akishughulika moja kwa moja na masuala ya rasilimali madini na haki za wachimbaji,

· Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Tawi, akishiriki kupanga na kusimamia ajenda za maendeleo kwa msingi wa kisera na kimkakati,

· Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Wazazi Wilaya ya Shinyanga DC, nafasi ambayo bado anaendelea kuitumikia kwa bidii na uaminifu.

· Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Vijijini, nafasi ambayo bado anaendelea kuitumiakia kwa bidii hadi sasa katika kutekeleza sera za cahama cha Mapinduzi CCM.

· Mkurugenzi kampuni ya Fadson General Company Limited.

·Mpaka sasa ni mkulima na mchimbaji wa madini ya dhahabu, mwekezaji wa sekta ya madini ya dhahabu Shinyanga vijijini.




from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/SORzsdP

No comments