WALICHOKIFANYA WANANCHI WA WILAYA YA MULEBA KWA WALIOTEULIWA KUGOMBEA NAFASI YA UBUNGE JIMBO LA MULEBA KASKAZINI NA KUSINI
Wananchi wa Jimbo la Muleba Kasikazini baada ya kumpokea ndugu Adonis Bitegeko mteuliwa nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini
Bwana Adonis Bitegeko aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kasikazini akizungumza baada ya kufika ofisi za chama cha Mapinduzi (CCM)
Na Mariam Kagenda _Kagera
Wananchi wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamejitokeza kwa wingi uwanja wa Ndege Bukoba kuwapokea walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi kugombea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Muleba Kusini na Muleba Kaskazini wilaya ya Muleba mkoani Kagera .
Wananchi hao baada ya kuwapokea wateuliwa wa nafasi hiyo ambao ni Adonis Bitegeko aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini na Dkt. Oscar Kikoyo Jimbo la Muleba Kusini waliwasindikiza kwa msafara wa magari na pikipiki mpaka kwenye ofisi za chama cha mapinduzi .
Baada ya Wagombea hao kufika ofisi za Chama hicho wameishukuru halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwa imani yao kubwa ya kuwateuwa kugombea nafasi ya Ubunge katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika October 2025 na Wananchi ambao waliwachagua kwa kura nyingi katika uchaguzi wa Kura za maoni .
Leo Agosti 25 watachukua fomu za kugombea nafasi ya Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 2025 .
Ikumbukwe kuwa Adonis Bitegeko ndiye aliyeongoza katika Uchaguzi wa kura za maoni kwa Jimbo la Muleba Kasikazini kwa kupata kura 4392 na Dkt Oscar Kikoyo aliongoza kwa kupata kura 4710 .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Muleba Athumani Kahara amewahimiza wanachama wa chama hicho kuvunja makundi kwani kwa sasa kilichobaki ni kuwanadi Wagombea walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi na kuhakikisha wanatafuta ushindi wa kishindo wa Chama hicho.
Aidha amesema kuwa watafanya Kampeini za kistaarabu za kuhakikisha wanailinda amani na kujiepusha na vitendo vyote vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani katika kipindi cha Uchaguzi mkuu .


Wananchi wa wilaya ya Muleba wakiwa uwanja wa Ndege kuwasubiri wateuliwa
Wananchi wakimpokea Adonis Bitegeko aliyeteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Muleba Kaskazini
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/HmOi4bP
No comments