BALOZI MAPURI ASIFU MCHAKATO WA MAANDALIZI YA UCHAGUZI CHALINZE
Mh. Balozi, Omar Ramadhani Mapuri, Mjumbe wa Tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini
NA. ELISANTE KINDULU, CHALINZE
MJUMBE wa tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Mh. Balozi Omar Ramadhani Mapuri amesifu halmashauri ya Chalinze kwa mchakato wa maandalizi ya uchaguzi mkuu utakaoenda kufanyika Oktoba 29 mwaka huu nchini Tanzania.
Balozi Mapuli alitoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza wasimamizi wakuu na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo, kata na wa vituo vya kupigia kura katika semina ya wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi iliyifanyika jana katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugoba.
"Niwapongeze kwa kushiriki semina huku maandalizi mengine ya usimamizi yakienda vizuri. Ila kufanikisha yote hayo ni kuzingatia mafunzo ambayo utekelezaji wake ni siku ya uchaguzi Oktoba 29", alisema balozi Mapuri.
Naye Mratibu wa Uchaguzi mkoa wa Pwani Bw. Gelard Busori aliwapongeza washiri wa mafunzo hayo kwa kupata fursa ya kuteuliwa na hivyo kuwataka kuifanya kazi hiyo ya usimamizi kwa weledi mkubwa.
Akifungua mafunzo hayo, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Chalinze Bwana Jovin Bararata amewasisitiza wasimamizi wa vituo na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura kuzingatia sheria, miongozo na maadili katika kazi yao watakapokuwa wakiwahudumia wapiga kura siku ya uchaguzi.
"Mnapokuwa kwenye vituo vya kupiga kura mfanye kazi kwa team work, mzingatie katiba, miongozo bila kusahau lugha ya staha na mavazi ya haiba", alisema Bw. Bararata.
Jimbo la Chalinze lina vituo vya kupigia kura 631 katika kata 15.


from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/OoSPC9Q










No comments