Na Michael Abel.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA) imeadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa kufanya hafla maalum katika ofisi zake, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa wafanyakazi wake na kuimarisha utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hafla hiyo imefanyika leo Ijumaa Oktoba 10 2025, katika ofisi za SHUWASA Shinyanga Mjini na kuudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro, ambapo mali na mengi yaliyofanyika, mfanyakazi bora amezawadiwa zawadi kwa kujituma na kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na ubunifu.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, amewataka watumishi wa SHUWASA kuendelea kutoa huduma zenye ubora na kuwaheshimu wateja, akisisitiza kuwa serikali inatambua umuhimu wa huduma bora kama nguzo ya maendeleo na ustawi wa wananchi, na kuwa mamlaka za maji zinapaswa kuwa mfano wa nidhamu, uwajibikaji na ubunifu katika kuhudumia jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa SHUWASA, Mhandisi Yusuph Katopora, amewapongeza wafanyakazi wote kwa kujituma katika kazi na kutoa huduma bora, huku akiwashukuru wananchi kwa kuendelea kuiamini mamlaka hiyo. Amesema SHUWASA itaendelea kuboresha miundombinu na mifumo ya utoaji huduma ili kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama kwa wakati wote.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Shinyanga wameipongeza SHUWASA kwa huduma bora na utayari wa kushughulikia changamoto kwa haraka, Wamesema mamlaka hiyo imekuwa mfano wa uwajibikaji na imechangia kuboresha maisha ya wakazi wengi kupitia upatikanaji wa maji safi na huduma za usafi wa mazingira, hali inayoongeza imani kwa wananchi kuendelea kushirikiana nayo.
<<<TAZAMA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI>>>





























from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/w2VsOhM
No comments