Nchi ya Burundi yapatiwa Ikulu Mpya na China
Balozi wa China nchini Burundi, Li Changlin na Waziri wa Mambo ya nje wa Burundi, Ezechiel Nibigira wamesaini hati ya makabidhiano ya jengo la Ikulu ya Burundi lililojengwa kwa msaada wa China.
Waziri wa mambo ya nje wa Burundi, Nibigira ameishukuru China kwa kujenga Ikulu hiyo, ambayo Burundi haijawahi kuwa nayo tangu ijipatie uhuru mwaka 1962, na kusema kwamba hii ni mara ya kwanza katika historia kwa Burundi kupata miundombinu mizuri, na imethibitisha uhusiano imara wa kisiasa na kidiplomasia uliopo kati ya Burundi na China.

No comments