Breaking News

Manchester United kuwakosa nyota wake 10 dhidi ya Crystal Palace

Klabu ya Manchester United inaweza kuwakosa wachezaji wake 10 katika mchezo wa Jumatano dhidi ya Crystal Palace kwasababu ya kuwa majeruhi.

United ililazimika kuwatoa wachezaji wake Ander Herrera, Juan Mata na Jesse Lingard kwenye mchezo wa Jumapili dhidi ya Liverpool katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo ulioisha kwa sare ya bila kufungana pia ilipelekea Marcus Rashford kuendelea na mchezo japo alikua na tatizo kwenye enka.

Nemanja Matic na  Anthony Martial wote waliukosa mchezo dhidi ya Liverpool wakati Phil Jones, Matteo Darmian, Antonio Valencia na Mason Greenwood pia hawakuweza kushiriki kutokana na kuwa majeruhi

kwa hali hii inamfanya kocha wa Manchester United kuwa na kikosi kidogo kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Crystal Palace kwenye dimba la Selhurst Park.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2GMB5xH

No comments