Breaking News

Rais Mstaafu Kikwete amlilia Ruge Mutahaba


Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza kuguswa na kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group (CMG), Ruge Mutahaba.

Dkt. Kikwete ameeleza kuwa Ruge alimsaidia mengi kipindi cha uongozi wake kwani alikuwa ni kijana mzalendo wa kweli. kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ameandika;

"Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo cha Ruge Mutahaba. Taifa limepoteza kijana wake mahiri, mbunifu na mzalendo wa kweli," ameeleza.

"Nimepoteza rafiki, mshirika mwaminifu na mtu ambaye amenisaidia kwa mengi katika uongozi wangu na hata baada ya kustaafu. Moyo wangu uko pamoja na wazazi wake, ndugu zake na familia yake katika kipindi hiki kigumu. Namuombea kwa Mola ampe Mapumziko Mema Peponi, Ameen," ameeleza Dkt. Kikwete.

Ruge Mutahaba amefariki dunia siku ya jana nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, Ruge atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika tasnia ya muziki nchini.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2GNTydu

No comments