Breaking News

Mkuu wa mkoa wa Mtwara aomba pombe aina ya Gongo kuhalalishwa


Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria kufanya marekebisho ya sheria ya pombe za kienyeji ili kuihalalisha.

Hatua hiyo ni baada ya kupokea majibu ya sampuli iliyochukuliwa kwenye pombe aina ya Gongo inayozalishwa kutoka kwenye bibo, kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, na kuthibitika kuwa inaweza kutumika kuzalisha spiriti iwapo itafikishwa viwandani.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2JzHPyt

No comments