SHANGWE ZATAWALA KITUMBO AKIREJESHA FOMU UTEUZI KUWANIA UDIWANI KATA YA MJINI - SHINYANGA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Salum Shabani Kitumbo amerudisha Fomu za uteuzi kugombea Udiwani Kata ya Mjini Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Amerudisha Fomu hizo leo Agosti 27,2025 kwa msimamizi msaidizi wa Uchaguzi (INEC) Kata ya Mjini Simon Mashishanga, huku akisindikizwa na wanachama wa CCM.
Kitumbo akizungumza mara baada ya kurudisha Fomu hizo,amesema anakishukuru Chama chake kwa kumuamini na kupitisha jina lake kugombea nafasi hiyo ya Udiwani Kata ya Shinyanga Mjini,na kuahidi ataitendea haki katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Aidha,ameomba makundi yote yaliyokuwepo wakati wa kura za maoni za kumtafuta mshindi mmoja wa kugombea nafasi hiyo ya udiwani,kwamba yavunjike na kuungana kuwa kitu kimoja na kutafuta kura za ushindi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025 kwa nafasi za Udiwani,Ubunge na kura nyingi za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/u9esqcG
No comments