DC MASINDI AWATAKA WAGOMBEA KUTUMIA JUKWAA KUFANYA SIASA ZA HESHIMA NA SIO MATUSI

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Tarafa ya Mondo Agosti 27,2025
Na Sumai Salum-Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi amewataka wagombea wote wa Jimbo la Kishapu wanaoelekea kuanza kampeni za uchaguzi kutumia lugha ya heshima na sera zenye kujenga badala ya matusi au kejeli wanapokuwa jukwaani.
Akizungumza Agosti 27, 2025 katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Tarafa ya Mondo,Masindi amesema siasa za matusi hazina tija, na kuwakumbusha wagombea kwamba kuna maisha baada ya uchaguzi, hivyo hakuna sababu ya kuchochea uhasama.
“Wananchi wanataka kusikia sera zinazogusa maisha yao na namna mtakavyoboresha huduma za kijamii. Huu sio muda wa matusi wala kejeli. Tufanye siasa zenye heshima na staha,” amesema Masindi.
Aidha, amewataka wananchi kusikiliza kwa makini sera za wagombea na kufanya maamuzi sahihi ifikapo Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa msingi wa maendeleo upo mikononi mwao. Vilevile, Masindi amewahimiza wananchi kuendelea kuchangamkia fursa za kiuchumi, kufanya kazi kwa bidii, kuishi kwa nidhamu na kumtanguliza Mungu katika kila jambo.

Afisa Tarafa ya Mondo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Atka Faki akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Agosti 27,2025
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wazazi pia kuhakikisha wanalea watoto wao kwenye maadili, nidhamu na ujasiri ili wawe nguzo ya maendeleo ya jamii.
Katika wito wake kwa jamii, amewahimiza kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo ikiwemo uanzishaji wa maboma ya madarasa, nyumba za walimu, vituo vya afya pamoja na kulinda miundombinu ya maji na umeme iliyowekwa kwa manufaa ya wananchi.
Mbali na hayo, amewahimiza watendaji wa Halmashauri na wakuu wa taasisi zingine za Umma na za fedha kuhakikisha wanafanya kazi kwa maslahi ya wananchi na kuwasogezea huduma muhimu ambazo serikali imekusudia kuwafikishia.
Aidha, wananchi wameelimishwa kuhusu huduma za mikopo zinazotolewa na Halmashauri na Taasisi ya Kifedha (CRDB), huku wakihimizwa kuchangamkia fursa hizo ili kuepuka kuingia kwenye mikopo isiyo rasmi inayochochea migogoro ya kifamilia.
Mhe.Masindi amehitimisha ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika tarafa ya Mondo Vijiji vya Nyasamba Kata ya Bubiki, Mwajiningu Kata ya Busongwa,Itongoitale Kata ya Mwasubi pamoja na Kijiji cha Idukilo Kata ya Idukilo.



Afisa wa taasisi ya fedha CRDB tawi la Maganzo Benjamini Sheka akitoa elimu ya fedha na mikopo kwenye mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi wa kupokea na kutatua kero za wananchi Agosti 27,2028

















Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwajiningu Kata ya Busangwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga James Daniel akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Agosti 27,2025

Mwenyekiti wa Kijiji chaItongoitale Kata ya MwasubiWilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Furahisha Jilinga akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Agosti 27,2025

Mwenyekiti wa Kijiji cha Idukilo Kata ya Idukilo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Patrick Kapela Mabala akifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi Agosti 27,2025




from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/03se5DZ
No comments